The House of Favourite Newspapers

Bodaboda Wapewa Sare Zitakazowatambulisha Kukabiliana Na Uhalifu

Katika kuhakikisha matukio ya uhalifu yanayotekelezwa na baadhi ya waendesha pikipiki, Mkaguzi Kata ya Kati Jijini Arusha Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Hamis Ally amegawa sare (viakisi mwanga) kwa bodaboda wa kituo cha Geti la Kuku katika kata hiyo kwa ajili ya kutambulika wakati wakiendelea na shughuli zao.

Mkaguzi huyo amefikia uamuzi huo ikiwa ni mkakati wake wa kuhakikisha bodaboda wote katika Kata hiyo wanatambulika kwa kuwa na sare maalumu ambazo zitakua zinawatambulisha sehemu popote watakapokuwa wanaenda.

Aidha amewaasa madereva wa bodaboda katika kata hiyo kutoshiriki matendo ya uhalifu ikiwemo usafirishaji wa dawa za kulevya, mauaji na uporaji wa vitu mbalimbali huku akisisitiza atakayematwa akishiriki matendo hayo atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kituo hicho Bwana Joseph Laizer amemshukuru na kumpongeza Mkaguzi huo kwa kuwapatia sare hizo ambapo amebainisha kuwa zitawafanya watambulike wakati wote kwani baadhi ya wahalifu hutumia pikipiki kutekeleza matukio ya uhalifu huku wakijifanya ni waendesha bodaboda.

JUMA AMWAGIWA PETROLI na KUCHOMWA MOTO HADI KUFARIKI – “MKE ALIMWAGA MAFUTA -MUME AKAWASHA KIBERITI”