The House of Favourite Newspapers

Bodi ya Barabara Mkoa wa Dar yakutana

0

1 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, akizungumza jambo. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara, Mussa Azzan Zungu.

2Kikao kikiendelea ukumbi wa Karimjee.

3Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Barabara na wanahabari wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick,  leo ameongoza kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa kilichojumuisha wakuu wa wilaya, wabunge na wataalam wa sekta ya barabara ili kusisitiza uratibu, ushauri na ufuatiliaji wa miundombinu ya barabara za mkoa huo.

Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam ambapo alisema kikao hicho ni cha kwanza baada ya uchaguzi mkuu wa 2015 kukamilika na akawapongeza baadhi ya wabunge waliohudhuria kikao hicho kwa kuchaguliwa kwao.

 “Mkoa wetu ni mdogo lakini unayo mahitaji makubwa ya miundombinu ambayo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mtandao finyu wa barabara usiotosheleza mahitaji kwani idadi ya magari inayoongezeka kila siku ni kubwa mno na hivyo kusababisha msongamano  wa magari katika barabara chache zilizopo,” alisema.

Aidha alisema kikao hicho kitakuwa na dondoo mbalimbali ikiwemo kupata taarifa ya utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa katika vikao vilivyopita na kupokea taarifa ya ziara ya wajumbe wa bodi wa wilaya zote tatu waliotembelea  miundombinu ya wilaya zote.

Alitaja  bajeti iliyotengwa ya fedha za matengenezo ya barabara kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2015/2016 kuwa ni  76,886,224,796/= ambapo jumla ya 93,181,990/= zitapelekwa katika Halmashauri ya Jiji la Dar.

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala  imetenga 11,000,950,000/= kwa kukarabarati miundombinu na  Kinondoni jumla ya 14,130,449,581/=   Manispaa ya Temeke imetenga 5,416,767,225  ambapo wakala wa barabara (TANROADS) Mkoa wa  Dar es Salaam ni 46,244,886,000/=.

Na Denis Mtima/Gpl

Leave A Reply