The House of Favourite Newspapers

Bodi ya Filamu Nchini Yazungumzia Ukuaji Wake

2.Kutoka kushoto ni Ofisa Habari wa Idara ya Habari (Maelezo), Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu, Joyce Fisso na Kaimu Mkuu wa mawasiliano Wizara ya Habari,Utamaduni na Michezo, Genofeva Matemu.
Kutoka kushoto ni Ofisa Habari wa Idara ya Habari (Maelezo), Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu, Joyce Fisso akifuatiwa na Kaimu Mkuu wa Mawasiliano  katika Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Genofeva Matemu.

3.Wanahabari wakifuatilia mkutano huo.Wanahabari wakifuatilia mkutano huo.

BODI ya Filamu  nchini imezungumzia namna ilivyopata mafanikio yake kwa kipindi cha mika ya 2014/15.

Akizungumza na wanahabari leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Wizara ya Habari na Vijana, Utamaduni na Michezo, Genofeva Matemu,  amesema kuwa hiyo ni taasisi ya serikali iliyoundwa kwa mujibu wa sheria ya filamu na michezo ya kuigiza kifungu Na. 4 cha mwaka 1976.

Amesema tasnia ya filamu na michezo ya kuigiza ina mchango mkubwa katika kuleta maendeleo hapa nchini na kupunguza umaskini.

Aidha ameendelea kutoa ufafanuzi kuwa vijana pamoja na makundi mengine yamefaidika kupata ajira kutoka katika shirika la Milki Bunifu Ulimwenguni ambalo  liliripoti kuwa mwaka 2007 tasnia ya filamu iliajiri watu 36 na mwaka wa fedha 2014/15 taarifa zikionesha sekta ya filamu iliajiri wataalam 944 na wadau 731,737, hivyo kufanya jumla ya watu 732,681 kupata ajira kupitia tasnia ya filamu.

NA DENIS MTIMA/GPL

Comments are closed.