Bodi ya Wakurugenzi Simba SC Yatangaza kamati Rasmi ya Uchaguzi
BODI ya wakurugenzi wa klabu ya Simba imefanya uteuzi wa kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo ambayo itahusika na kuandaa na kusimamia uchaguzi mkuu wa klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Msimbazi jijini Dar es Salaam.
Kamati hiyo inaongozwa na Mwenyekiti Mh. Boniface Lihamwike akiwa na Makamu Mwenyekiti wake Wakili Mwajuma Choggy pamoja na wajumbe watatu ambao ni Richard Mwalibwa, Gerald Mongela pamoja na Juma Simba.
Kwa mujibu wa taarifa ilyotolewa na Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba kupitia kurasa rasmi ya mtandao wa kijamii wa Instagram imebainisha kuwa wateule hao wataanza kazi mara moja baada ya uteuzi.