Boko Haram Wakiri Kuua Wakulima

KIONGOZI wa kundi la Boko Haram, Abubakar Shekau, amesema kundi lake ndilo lililohusika na mauaji ya wakulima 78 katika eneo la Zabarmari jirani na Maiduguri, kaskazini-mashariki mwa Nigeria mwishoni mwa wiki iliyopita.

 

Katika mkanda wa video uliorekodiwa na kusambazwa na kundi hilo, kiongozi huyo akiwa amejiziba uso wake, anasikika akikiri kwamba kundi la Boko Haram ndilo lililofanya mauaji hayo nchini Nigeria.

 

Wakati kundi hilo likikiri kuhusika na tukio hilo, wabunge wa Nigeria wamefanya mazungumzo na Rais Muhammadu Buhari na kuitaka serikali kuyachukulia kwa uzito mauaji hayo dhidi ya raia wasio na hatia.

Toa comment