The House of Favourite Newspapers

Bombadier 2 ‘Zaibwa’ Uwanja wa Ndege Lagos

 

Murtala Muhammed International Airport (MMA).

NDEGE mbili aina ya Bombardier Dash 8 Q300 zilizokuwa zinamilikiwa na kampuni ya Topbrass Aviation Services Limited, zimedaiwa kuibwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Murtala Muhammed wa Lagos, Nigeria.

Ndege hizo zenye usajili wa 5N-TBB na 5N-TBC, ziko katikati ya mpambano wa kisheria kati ya mkodishaji, Seagold Investment Limited, na Topbrass Aviation Services.

Uchunguzi uliofanyika umeonyesha kwamba ndege hizo zimehamishwa mahali zilipokuwa zimeegeshwa katika uwanja huo na kupelekwa kwenye banda la kampuni ya  Aero Contractors’ Maintenance and Overhaul (AMO) ambapo namba tayari zimefutwa na kwa sasa zikifanyiwa matengenezo ili ziondolewe Lagos na kupelekwa sehemu ambayo haijajulikana.

 

Image result for Unease over ‘stolen’ jets at Lagos airport

Sehemu ‘zilikofichwa’ ndege hizo.

Comments are closed.