The House of Favourite Newspapers

Bomoa Bomoa Yapitia Kituo cha Mafuta cha GAPCO Kilichopo Kamata, Dar

DAR ES SALAAM: Sehemu ya Kituo cha Mafuta cha Gapco kilichopo eneo la Kamata jijini Dar es Salaam, kimebomolewa mapema leo kwa kile kilichoelezwa kuwa kipo ndani ya eneo la reli.

 

 

Zoezi hilo ambalo limeanza asubuhi ya leo, limeendeshwa na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) dhidi ya watu waliofanya maendelezo ya ujenzi ndani ya eneo la reli hiyo.

Huu ni mwendelezo wa bomoa bomoa katika Jiji la Dar es Salaam kwa wale waliojenga katika hifadhi ya reli. Hivi karibuni kulishuhudiwa nyumba za wakazi wa Buguruni na majengo ya wafanyabiashara katika eneo hilo yakibomolewa ili kupisha ujenzi wa reli ya treni ya kisasa, reli ambayo inatarajiwa kuanza kujengwa hivi karibuni kuelekea Morogoro hadi Dodoma.

Comments are closed.