The House of Favourite Newspapers

Bomoabomoa Mbezi Beach Acha Kabisa!

0

1.Wakazi wa maeneo ya mbezi bichi wakishudia zoezi la bomoabomoa.Wakazi wa maeneo ya Mbezi Beach wakishudia zoezi la bomoabomoa.

2.Mwonekano wa nyumba ya gorofa moja kabla haijabomolewa.Mwonekano wa nyumba ya gorofa moja kabla halijabomolewa.

3.Tingatinga likianza zoezi la kubonmoa fensi ya nyumba hiyo kabla ya zoezi la kuanza kubomoa nyumba yenyewe.Tingatinga likianza zoezi la kubomoa fensi ya nyumba hiyo kabla ya zoezi la kuanza kubomoa nyumba yenyewe.

4.Baadhi ya vitu vilivyokuwemo ndani vikiwa vimetolewa.Baadhi ya vitu vilivyokuwemo ndani vikiwa vimetolewa.

5.Zoezi la kubomoa nyumba hiyo likiwa limeanzaZoezi la kubomoa nyumba hiyo likiwa limeanza.

6.Ulinzi ukiwa umeimalika vya kutosha eneo hilo.Ulinzi ukiwa umeimarika vya kutosha eneo hilo.

7.Mama mwenye nyumba aliyedaiwa kuvamia kiwanja cha mtu.Mama mwenye nyumba aliyedaiwa kuvamia kiwanja cha mtu.

8.Wanaoonekana kusimamia zoezi hilo ni (nyuma ya tingatinga ni) maofisa kutoka manispaa ya kinondoni.Wanaoonekana kusimamia zoezi hilo (nyuma ya tingatinga ) ni maofisa kutoka manispaa ya kinondoni.

9.Baadhi ya vijana wakisaidia kuondoa vitu vilivyokuwemo ndani ya nyumba hiyo.Baadhi ya vijana wakisaidia kuondoa vitu vilivyokuwemo ndani ya nyumba hiyo.

10.Zoezi la kutoa vitu ndani likiendelea.Zoezi la kutoa vitu ndani likiendelea.

MANISPAA ya Kinondoni jijini Dar es Salaam ikishirikiana na Wizara ya Ardhi  inaendelea na oparesheni maalum ya kubomoa nyumba zilizojengwa kinyume na sheria katika manispaa yake. Oparesheni hiyo jana ilitinga maeneo ya Mbezi Beach na kuibomoa nyumba iliyokuwa Mtaa wa Libermann.

Kamera ya Global ilipita maeneo hayo na kujionea zoezi hilo likitekelezwa kwa kutumia gari la ‘tingatinga’ likivunja jengo lililojengwa kinyume na sheria mtaani hapo ambalo mmiliki wake alitajwa kwa jina moja la Deus na mkewe akijitambulisha kwa jina la Catherine waliodaiwa kuvamia eneo hilo na kujenga nyumba.

Kwa mujibu wa maofisa hao wa manispaa ya Kinondoni waliokuwa wakisimamia zoezi hilo la bomoabomoa walisema kuwa, mtu huyo alijenga nyumba kinyume na sheria kwani mmiliki halali wa kiwanja hicho yupo, hivyo zoezi litaendelea kwa wale wote waliojimilikisha ardhi na kujenga sehemu zilizo wazi (open spaces).

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply