The House of Favourite Newspapers

Bondia Anthony Joshua Ashinda Kwa KO vs Wladimir Klitschko Uwanja wa Wembley (Video)

0
Anthony Joshua wa Uingereza akishangilia baada ya kumtwanga mpinzani wake roud ya 11 kati ya 12 bondia Wladimir Klitschko (hayupo pichani) wa Ukraine katika pambano la uzito wa juu katika Uwanja wa Wembley.

Mbambano ukiendelea Anthony Joshua wa Uingereza (kushoto) na Wladimir Klitschko wa Ukraine (kulia).

Anthony Joshua akiwa chini kwa mara ya kwanza baada ya kutupwa konde zito na Klitschko.

Anthony Joshua wa Uingereza usiku wa kuamkia leo aliingia ulingoni katika Uwanja wa Wembley kupambana na bondia Wladimir Klitschko wa Ukraine katika pambano la uzito wa juu.

Pambano hilo ambalo Joshua mwenye umri wa miaka 27 alimpiga kwa KO round ya 11 kati ya 12 Wladimir Klitschko mwenye umri wa miaka 41  na mataji ya IBF, WBA na IBO katika uzito wa juu.
Joshua ana umri wa miaka 27 tu lakini anaonekana ni miongoni mwa mabondia hatari katika uzito wa juu kwani hadi sasa amepigana mapambano 19 na kushinda yote, tena kwa Knock Out yaani ‘KO’.

Leave A Reply