Bondia Mkongwe George Foreman Afariki Dunia

Bingwa wa mara mbili wa mkanda wa dunia wa uzito wa juu na mshindi wa medali ya dhahabu ya Olimpiki, bondia George Foreman, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 76.
Miongoni mwa mambo mengi yaliyompa umaarufu miaka mingi nyuma, ni pambano la Rumble in the Jungle alilopigana na Muhammad Ali, ambapo alimpa upinzani mkubwa ambao haukutarajiwa.
Ukurasa rasmi wa familia ya Foreman kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram umeandika:
“Mioyo yetu imevunjika. Kwa huzuni kubwa, tunatangaza kifo cha mpendwa wetu George Edward Foreman Sr., ambaye alifariki kwa amani mnamo Machi 21, 2025, akiwa amezungukwa na wapendwa wake.
“Mhubiri mwaminifu, mume mpendwa, baba mwenye upendo, na babu pamoja na babu mkubwa anayejivunia, aliishi maisha yaliyojaa imani thabiti, unyenyekevu, na malengo.
“Akitambulika kama mmoja wa wapiganaji wenye nguvu zaidi katika historia ya ndondi, Foreman alishinda dhahabu ya Olimpiki katika pambano lake la 25 pekee kama bondia wa ridhaa, akamshinda mmoja wa mabondia bora wa wakati wote, Joe Frazier.
“Kisha akashikilia taji la uzito wa juu mara mbili kabla ya pambano lake maarufu la mwaka 1974 dhidi ya Ali huko Kinshasa, Zaire—ambayo sasa inajulikana kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.