Bondia wa Kimataifa Afariki kwa Kipigo

BONDIA raia wa Urusi, Maxim Dadashev,  amefariki dunia baada ya pambano lake dhidi ya mpinzani wake, Subriel Matias,  kumsababishia majeraha makubwa ya ubongo.

Dadashev mwenye umri wa miaka 28, alishindwa kuendelea na pambano hilo ambalo mkufunzi wake, Buddy McGirt, alilazimisha lisimamishwe katika raundi ya 11 baada ya bondia huyo kupokea kichapo kikali.

Pambano hilo lilipigwa Julai 20, 2019, ambapo baada ya pambano Dadashev alikimbizwa hospitali na madaktari walimfanyia vipimo na kugundua kuwa damu ilikuwa ikimvuja kwenye ubongo na kufanyiwa operesheni ya saa mbili, ambapo jana Jumanne alipoteza maisha.


Loading...

Toa comment