The House of Favourite Newspapers

Bonga Aachana na Harmonize, Atimkia Lykos Empire – Video

0
Mkurugenzi Mtendaji wa Lykos Empire, Dion Machum Charles (kushoto) akizungumza baada ya kutiliana saini na Bonga.

Prodyuza wa Harmonize almaarufu kwa jina la Bonga leo ametangaza rasmi kuachana na msanii huyo na kujiunga lebo ya Lykos Empire ambapo ataendelea kuwa prodyuza na muimbaji.

Bongo akitia saini mkataba wa kufanyakazi na Lykos Empire.

Akizungumza na wanahabari kwenye mkutano uliofanyika Hoteli ya King D, leo mchana Bonga amesema sababu kubwa iliyomuahamisha ni kutafuta maslahi ya kimaisha.

Prodyuza Bonga akizungumza na wanahabari ( hawapo pichani) baada ya kutiliana saini na Lykos Empire

Akijibu maswali ya wanahabari Bonga alikanusha kuondoka kwa Harmonize baada ya kutofautiana nae na kusistiza kuwa lengo kubwa la kuhama ni kupanua mawazo na kusaka maslahi zaidi.

Sehemu ya wanahabari walikuwa kwenye mkutano huo.

HABARI:NEEMA ADRIAN PICHA: RICHARD BUKOS/GPL

BONGA Asema UKWELI Kilichomtoa kwa HARMONIZE / MALIPO, NYIMBO Alizoacha..

Leave A Reply