The House of Favourite Newspapers

Bongo Fleva yashinda kwa taabu mbele ya Global FC – VIDEO

Kikosi cha Global FC kilichocheza na Bongo Fleva katika Uwanja wa Shule ya Msingi Vikawe, Kibaha.

BONGO Fleva juzi ijumaa ilichafua rekodi ya Global FC baada ya kuishinda kwa mbinde kwa penalti 4-2 Mechi hiyo ilipigwa katika Uwanja wa Shule ya Msingi Vikawe, Kibaha, huku dakika tisini zikimalizika kwa suluhu ambapo refa aliamuru penalti zipigwe ili mshindi aweze kupatikana.

Kikosi cha Bongo Fleva

Mabao ya penalti za Bongo Fleva yalifungwa na M2 tha P, Rich One, Mansulee na Foby huku zile mbili za Global FC iliyokuwa bila mastaa wake kibao ambao wengine wamekwenda kwenye majaribio, zikifungwa na Omary Mdose pamoja na Richard Kibona.

Miongoni mwa mastaa wa Global ambao wako nje kwa majaribio ni pamoja na Philip Nkini, Saleh Ally, Lunyamadzo Mlyuka na Ibrahim Mressy.

Comments are closed.