The House of Favourite Newspapers

Bongo Fleva yataja kikosi cha kuimaliza Global FC

TIMU ya wasanii wa Bongo Fleva imeweka hadharani listi ya wasanii wao ambao itawashusha uwanjani leo Ijumaa katika mechi ya kirafiki dhidi ya Global FC itakayofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Vikawe wilayani Kibaha.

 

Akizungumza na gazeti hili, nahodha wa Bongo Fleva, Rich One alisema kuwa wasanii wote wa Bongo Fleva ambao wanaunda sehemu ya kikosi hicho watakuwepo na hakuna taarifa za majeruhi wala za mchezaji yeyote atakayekosa mchezo huo hivyo watuwajitokeze kwa wingi.

“Mimi kama nahodha mpaka sasa sina majeraha, watu wajitokeze kwa wingi kwani nitakuwa na wachezaji wangu wote akiwemo Stamina, M2 Tha P, Abdu Kiba, Peter Manyika, Mchizi Mox, Jay Moe, T.I.D, Kalapina, James Tupatupa, Msaga Sumu, Mansu Lee, Papii Kocha, H Baba, Dully Sykes, Tunda Man, Soggy Dogy, Afande Sele, Amini, King Kapita na wengine pia. Aidha, kwa upande wa timu ya Global FC inayodhaminiwa na Kampuni ya Ashish Cinematography, kwa sasa imeweka kambi katika Hotel ya The Atriums kwa ajili ya kujiandaa na pambano hilo.

Comments are closed.