The House of Favourite Newspapers

BONGO MUVI KUMFUATA MSUKUMA DODOMA

 

WASANII wa filamu za Kibongo nchini wamesema wanajipanga kwenda jijini Dodoma kwa lengo la kumpongeza Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Kasheku ‘Msukuma’ kutokana na kupigania haki za wasanii wa tasnia hiyo.

 

 

Msukuma, juzi wakati akichangia Hotuba ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, aliwatetea wasanii akitaka haki zao zilindwe na serikali.

 

Msimamo huo umetolewa na Rais wa Shirikikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba leo Ijumaa, Aprili 19, 2019 katika Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam alipokutana na baadhi ya wasanii na wadau wa filamu.

 

 

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwakifwamba alisema: “Msukuma ameonyesha uzalendo mkubwa katika kuipigania tasnia ya filamu nchini, kwa hiyo sisi kama wasanii tumeona ipo haja ya kwenda Dodoma kumpongeza kwa kutujali wasanii.”

 

 

 

Lakini, walipouliza kuhusu kuingia ndani ya Bunge la Tanzania kumpongeza, Mwakifwamba alisema wakifika Dodoma ndipo taratibu nyingine za kuona ni namna gani wanaweza kuingia bungeni zitafuata.

 

 

Akifafanua zaidi Mwakifwamba amedai kuwa kwa asilimia kubwa Bodi ya Filamu inachangia kushusha tasnia hiyo nchini badala ya kuwatetea na kuondoa kodi zisizokuwa za msingi.

 

Mbali na Mwakifwamba, waigizaji wengine waliokuwepo ni Steve Nyerere, Chiku Mchome, Mzee Chilo, Jimmy Mafufu na wengine.

 

BONGO MUVI Waamua Kumfata MSUKUMA Bungeni “Kauli Imetuumiza”

Comments are closed.