The House of Favourite Newspapers

BONGO FLEVA, BONGO MUVI KUKIPIGA TAIFA JUMAPILI HII

Nahodha wa Bongofleva, Selemani Jabiri maarufu Msagasumu (wa pili kushoto) akizungumza kwa niaba ya wenzake. Kushoto ni msimamizi wa SG Sports, Amani Njeleka, na kulia kwake ni msanii wa Bongo Muvi, Vinceti Kigosi ‘Ray’ na Mike Sangu.

WASANII wa filamu nchini, Bongo Muvi na wa muziki, Bongo Fleva,  leo wamepewa vifaa vya michezo kwa ajili ya mechi yao ya soka itakayopigwa Uwanja wa Taifa, Dar Agosti 4 mwaka huu kabla ya Yanga kukipiga na Kariobang Sharks.

 

Wasanii hao wamepewa vifaa hivyo na kampuni ya SG Sports iliyopo Mikocheni mkabala na ofisi za Tanesco jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza baada ya kukabidhi vifaa hivyo, msimamizi wa kampuni hiyo, Amani Njeleka, amesema wameamua kuwapa vifaa hivyo wasanii hao kwa ajili ya kusapoti sanaa ya muziki, filamu  na soka na kuahidi kuendelea kusapoti fani hizo.

 

Njeleka akimkabidhi jezi nahodha wa Bongo Muvi, Ray.

 

Msagasumu naye akikabidhiwa jezi kwa niaba ya wenzake.

 

Baada ya makabidhiano. 

PICHA: RICHARD BUKOS / GPL

Comments are closed.