The House of Favourite Newspapers

Boniface Mwabukusi achaguliwa kuwa Rais wa TLS – Video

0

Wanachama wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) wamemchagua wakili msomi Boniface Mwabukusi kuwa rais mteule wa chama hicho.

Wanachama wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) wamemchagua wakili msomi Boniface Mwabukusi kuwa rais mteule wa chama hicho.

Mwabukusi ametangazwa mshindi wa kiti hicho na Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mawakili Agosti 2, 2024.

Ni kwa kupata kura 1,274 ambazo ni sawa na asilimia 63.1 dhidi ya washindani wake Sweetbert Nkuba, Revocutus Kuuli, Ibrahim Bendera, Paul Kaunda na Emmanuel Muga katika uchaguzi ambao kwa mara ya kwanza umefanyika nje ya Jiji la Arusha.

Kinyang’anyiro cha uchaguzi huo kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC) jijini Dodoma, kililenga kumpata mrithi wa Harold Sungusia aliyemaliza muda wake.

Aidha,Mwabukusi ameibuka kidedea kwa kupata kura 1,274 mbele ya mgombea Sweetbert Nkuba aliyepata kura 807 ambapo jumla ya wapiga kura wote walikuwa ni 2,218 huku kura tatu zikiharibika.

Leave A Reply