Bonsi Vibe Festival Yafunika Dar Live (Picha+Video)

Mwanamitindo, muuza nyago na msanii wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto, akisalimia mashabiki kabla ya kutoa shoo usiku wa kuamkia leo ukumbi wa Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live,  uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

MASHABIKI wa burudani wa Bongo Fleva na Singeli, usiku wa kuamkia leo Agosti 13, 2019, katika kusherehekea Siku Kuu ya Idd walipata bonge la burudani kwenye Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar live katika Tamasha la Bonsi ambalo lilikuwa noma saaana aisee.

 

Wasanii  ambao wametoa burudani ni mwanamitindo, muuza nyago na msanii wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto, mtaalam wa Singeli Mzee wa Bwax, Easy Man na wakongwe wa Bongo Fleva, Chid Benz na Mr Blue wakisindikizwa na mkali wa kupuliza matarumbeta, Kiroboto OG .

Mashabiki wakiangalia shoo ya Hamisa Mobeto (hayupo pichani)

Mpango mzima ulianza na matarumbeta ya Kiroboto OG kisha mkali wa singeli, Eazy Man, kupanda jukwaani naye kufuatiwa na  mkali mwingine wa Singeli, Mzee wa Bwax, abapo alifunika ile mbaya.

Uhondo wa singeli ukiwa bado unasikiliziwa, mkali wa kuchana, Chid Benz, alivamia jukwaa na kufanya yake ambapo aliwateka mashabiki wa burudani waliokuwepo.

…Mobeto akifanya yake stejini.

Hayo yakiendele,a Hamisa Mobeto naye alivamia jukwaa na kuanza makamuzi ambapo mashabiki waliofurika ukumbini hapo ilikuwa ni full shangwe. Aliyemaliza kazi ukumbini hapo ni Mr Blue ambaye alipiga shoo ya aina yake.

Mashabiki wakigombania nguo ya Hamisa Mobeto (hayupo pichani) baada ya kuirusha kwa mashabiki.

Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Mr Blue, akitoa burudani.

Msanii anayetamba kwenye Singeli, Mzee wa Bwax,  akiongea na mashabiki wake.

Msanii wa Bongo Fleva, Rashid Makwiro, maarufu kwa jina la ‘Chid Benz’ akifanya yake.

Msanii wa muziki nchini, Ishaka Seseme,  maarufu kwa jina la Easy Man, akitoa burudani.

PICHA NA RICHARD BUKOS, GPL


Loading...

Toa comment