Boomplay Kusherehekea Wasanii wa Afrika Waliochaguliwa Kwenye Tuzo Za Grammy
Sekta ya muziki duniani inajitayarisha kwaajili ya usiku mkubwa wa mwaka kupitia tuzo za 65 za Grammy. Huku wasanii wa Kiafrika wakipokea teuzi za kihistoria katika kategori tofauti mwaka huu.
App inayokua kwa kasi katika utoaji huduma ya kupakua na kusikiliza muziki barani Afrika, Boomplay, imetangaza kampeni ya kusherehekea tukio hili.
Boomplay inawapa watumiaji wake subscription ya bure kufurahia na kugundua muziki bila vizuizi vyovyote na bila gharama kwa siku nzima, Jumatatu ya tarehe 6 Februari 2023, pale atakapotangazwa msanii yeyote wa Kiafrika kushinda katika kategori zao.
Afrika inajivunia teuzi nane katika hafla ya mwaka huu, na angalau msanii mmoja wa Kiafrika akitarajiwa kurudi nyumbani na tuzo hiyo ya Grammy, hivyo kuwafanya watumiaji wa Boomplay katika bara zima kusheherekea ushindi huo kupitia App hiyo.
Tosin Sorinola, Mkurugenzi wa Idara ya Wasanii na Mahusiano ya Umma Boomplay, amesema ”Boomplay imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono muziki na wasanii wa Kiafrika, na mpango wa subscription ya bure ni uthibitisho mwingine wa dhamira yetu ya kuendelea kuwezesha mfumo wa muziki wa Kiafrika.
Tunatoa subscription ya bure kwa watumiaji wetu wote kwa ajili ya kusherehekea ubora wa muziki wa Kiafrika katika tuzo za Grammy za 2023.
Kupitia subscription hii ya siku moja bila malipo, wapenzi wa muziki wanaweza kufurahia orodha yetu ya nyimbo zaidi ya milioni 90 ili kusikiliza maudhui bila matangazo na kupakua na kusikiliza bila bando, hii ni fursa nzuri kwa wapenzi wa muziki kuunga mkono na kusherehekea wasanii wanaowapenda. Tunajivunia kwa hatua kubwa zinazofanywa na wasanii wetu wa Kiafrika, kuuweka muziki wa Kiafrika kwenye ramani kimataifa, na hii ndiyo njia yetu ya kuwafurahia na kuwaunga mkono.”
Muziki wa Kiafrika uliwakilishwa vyema wakati Recording Academy ilipotoa orodha yake ya waliochaguliwa katika tuzo za 65 za Grammy. Mwimbaji nyota wa Nigeria Burna Boy na nguli wa Benin Angelique Kidjo wameteuliwa katika kipengele cha Albamu Bora ya Muziki ya Ulimwenguni, huku Rocky Dawuni wa Ghana, Eddy Kenzo wa Uganda, Wouter Kellerman wa Afrika Kusini, Zakes Bantwini na Nombeco Zikode na Burna Boy wote wakiwania kipengele cha Best Global Performance. Cha ajabu ni kwamba, nje ya kategoria za Global Music, Tems wa Nigeria ameteuliwa katika kipengele cha Utendaji Bora wa Kuimba kwa Melodic na Wimbo Bora wa Rap kwa ushirikiano wake na Drake na Future kwenye wimbo unaoongoza kwenye chati mbalimbali wa “Wait for You”.
Angelique Kidjo pia ameteuliwa katika kipengele cha Wimbo Bora uliowekwa kwenye kipengele cha Visual Media kwa Wimbo wake wa Woman King, “Keep Rising”.
Ikijulikana kwa vipengele vyake vilivyo rahisi kutumia na usikiliziaji wa muziki wenye sauti ya hadhi ya juu, Boomplay hutoa maktaba pana ya nyimbo na podikasti, pamoja na playlists zilizoratibiwa maalum kutoka kwa aina na wasanii mbalimbali, zinazosasishwa mara kwa mara ili kuhakikisha vibao vipya zaidi vinapatikana. Watumiaji wa Boomplay wanaweza kuunda orodha za kucheza, kugundua muziki mpya kupitia mapendekezo maalum, na kusikiliza nyimbo nje ya mtandao. Mfumo wa usikilizaji hutoa uchezaji wa nyimbo zilizopakuliwa bila matangazo na nje ya mtandao kupitia subscription ya bei nafuu kwa siku, wiki na mwezi na vifurushi vya bando kufuatia ushirikiano wake wa kimkakati na kampuni zinazohusiana za mawasiliano.
Kwa taarifa Zaidi kuhusiana na kampeni #BoomplayFreesubscription zinaweza kupatikana hapa: – https://www.boomplay.com/share/buzz/4162852