The House of Favourite Newspapers

Boomplay Yaingia Makubaliano na Halotel Kurahisisha Usikilizaji wa Muziki Kidijitali

0

 

Boomplay, App namba moja ya kusikiliza na kupakua muziki barani Afrika, Boomplay imeshirikiana na Kampuni ya Mawasiliano ya simu, Halotel kuzindua kifurushi cha ‘Boomplay na Halotel’ ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuendelea kurahisisha usikilizaji wa muziki kidijitali kwa Watanzania.

 

Ushirikiano huu unawapa fursa wateja wa Halotel kupata intaneti bila malipo na vifurushi vya kujiunga ili kusikiliza muziki bila kikomo wakiwa na uhuru wa kusikiliza maudhui ya kulipia Boomplay kwa bei iliyorahisishwa. Wateja wa Halotel wanaweza kupata vifurushi vya intaneti vya kila siku vya TZS 500/- na bonasi ya 100MB, bando la wiki la TZS 2,000/- na bonasi ya 300MB na bando la kila mwezi la TZS 6,000/- na bonasi ya 500MB.

 

“Ushirikiano huu ni hatua nyingine muhimu katika azma yetu ya kuhakikisha muziki unapatikana kwa urahisi zaidi kwa watanzania wote kupitia Mamilioni ya wateja wa Halotel, naamini ushirikiano wetu unatoa fursa nzuri ya kuwakaribisha wapenzi wa muziki karibu zaidi na nyimbo zao pendwa, podikasti na maudhui mengine mengi yaliyomo kwenye App ya Boomplay,” alisema Natasha Stambuli, Meneja Mkuu wa Boomplay Tanzania.

 

Akizungumzia ushirikiano huo, Mkurugenzi wa Biashara wa Halotel, Abdallah Salum alisema, “Kama moja ya watoa huduma wa intaneti yenye kasi zaidi nchini Tanzania, tunapenda kutumia fursa hii kuwapa wateja wetu vifurushi vya intaneti kwa bei nafuu kutoka mtandao wa Halotel ulioenea maeneo mengi nchini kwa kuwawezesha Watanzania kufurahia maisha ya kidijitali. Kupitia ushirikiano huu, wateja wetu sasa wanaweza kufurahia muziki wanaoupenda kupitia App ya Boomplay kwa kutumia vifurushi vinavyotoa thamani na urahisi.

 

 

Wateja wanaweza kufurahia usikilizaji bila matangazo na upakuaji bila kikomo wa mamilioni ya nyimbo kutoka kwa wasanii wanaowapenda kupitia App ya Boomplay kwa bei iliyorahisishwa baada ya kununua vifurushi vya Halotel Boomplay. Kwa wale ambao hawako kwenye mtandao wa Halotel wanaweza kupata laini ya Halotel kwenye maduka yao yaliyoko nchi nzima na kupakua App ya Boomplay ili kupata huduma hiyo.

 

 

Watumiaji wa Boomplay Halotel wanahimizwa kuboresha App yao ya Boomplay hadi toleo la hivi karibuni zaidi ili kufurahia matoleo mapya ya App.

 

 

Leave A Reply