The House of Favourite Newspapers

Bora Uchebe Afe Kuliko Kumkosa Shilole

Shilole na Uchebe.

 

MCHUMBA wa staa wa mduara Bongo, Zuwema Mohamed ‘Shilole’, Uchebe Ashiraf amefunguka kuwa kuliko kumkosa Shilole kwenye maisha yake ni bora asiwepo duniani kabisa.

 

Akipiga mastori na Over Ze Weekend, Uchebe alisema kuwa, pamoja na kwamba amegundua Shilole alirudisha mapenzi na bwana’ke wa zamani, Nuh Mziwanda lakini hayuko tayari kumuacha.

 

“Ninajua amenikosea sana, lakini siko radhi kumuacha, ninampenda mno na niko radhi kupoteza maisha yangu kwa ajili yake au niuze chochote nilichonacho ili tu nimridhishe atakavyo,” alisema Uchebe.

Na Imelda Mtema| Ijumaa Wikienda.

Comments are closed.