The House of Favourite Newspapers

Bosi Ajitokeza Kuimwagia Mamilioni Simba SC

0

 

NA WILBERT MOLANDI NA MUSA MATEJA | CHAMPIONI JUMAMOSI | DAR ES SALAAM

SIMBA msimu huu imecheza bila mdhamini kwenye jezi zake lakini wakimfuata Mkurugenzi wa Kampuni ya Bin Slum Tyres, Nassor Bin Slum kwa ajili ya kudhaminiwa, basi watarajie kumwagiwa mamilioni.

Tofauti na misimu iliyopita ilipokuwa ikidhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia Bia ya Kilimanjaro, Simba msimu huu imecheza ligi bila ya mdhamini wake mkuu ukiachana na wale wa Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Global TV Online kupitia kipindi cha Spoti Hausi, Bin Slum alisema anatamani kuzidhamini klabu kubwa za Simba na Yanga, lakini timu hizo zinataka fedha nyingi ndiyo sababu ya yeye kuachana nazo.

Bin Slum alisema, yeye yupo tayari kuidhamini timu kwa kiwango cha fedha cha Sh milioni 500 ambacho anaamini kwa Simba na Yanga ni ndogo kwani wenyewe hutaka udhamini wa Sh bilioni 1 ambazo ni nyingi kwake.

Aliongeza kuwa, kama timu hizo zitamfuata kwa ajili ya kuzidhamini, basi atafanya nazo mazungumzo kwa ajili ya kuzisaidia baada ya kuzidhamini Mbeya City, Stand United na Ndanda FC. “Mimi siyo shabiki wa Simba wala Yanga, mimi ni shabiki wa Coastal Union ya nyumbani kwetu Tanga.

“Sitakataa kama nikiombwa kuzidhamini klabu hizo kongwe za Simba na Yanga, nipo tayari logo ya biashara yangu iwekwe nyuma ya jezi chini na huko mbele wakawekwa wadhamini wakubwa.

“Nimesikitishwa na Simba kucheza ligi nzima msimu huu ya mdhamini wakati wadhamini wapo wengi na isitoshe ni klabu kubwa nchini,” alisema Bin Slum.

Leave A Reply