The House of Favourite Newspapers

Bosi GSM Apanda Ndege Kufuata Mashine Mbili Congo

0

YANGA sasa imeamua! Ndivyo utakavyoweza kusema ni baada ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na Usajili, Injinia Hersi Said, juzi kupanda ndege kufuata mashine mbili matata nchini DR Congo.

 

Hiyo ni katika kukiboresha kikosi hicho kinachojiandaa na Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa watakayoshiriki katika msimu ujao.

 

Yanga inaelezwa hadi hivi sasa tayari imefikia makubaliano mazuri na mabeki wawili ambao Shaban Djuma anayekipiga AS Vita na David Bryson wa KMC.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, Hersi amepanda ndege juzi kuelekea DR Congo kwa ajili ya kukamilisha usajili wa Djuma waliyefikia muafaka mzuri wa kusaini mkataba.

 

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, pia Hersi amekwenda huko kukamilisha usajili wa beki tegemeo wa FC Lupopo ambao huenda akatua nao kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyere (JNIA), Dar es Salaam baada ya kumalizana nao.

 

Aliongeza kuwa, wachezaji hao wanawasajili baada ya mapendekezo ya Kocha Mkuu wa timu hiyo, raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi.

 

“Hersi hayupo nchini kwa siku kadhaa, amesafiri kwenda Congo kwa ajili ya kukamilisha usajili wa Djuma na beki wa kati ambaye tegemeo hivi sasa kwenye kikosi cha Lupopo.“Kabla ya kwenda huko yalikuwa yamefanyika mazungumzo ya awali na wachezaji hao, hivyo amekwenda kumalizia dili hilo.

 

Kama mambo yakienda vizuri, upo uwezekano mkubwa wa wachezaji hao kuwasili nchini na tayari kujiunga na timu haraka, kwani hakutakuwa ya likizo ya wachezaji kama unavyofahamu kocha mpya, hivyo ni lazima aitengeneze timu kwa kukaa pamoja ili ‘pre-season’ iwe nzuri,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Hersi hivi karibuni alisema kuwa: “Tumepanga kufanya usajili utakaokuwa tishio kimataifa, usajili huo tumepanga kuufanya kwa siri kubwa.“Usajili huo utamuhusisha kocha wetu Nabi ambaye atatoa mapendekezo ya usajili wa wachezaji wote na wale wa zamani ambao angetaka kufanya nao kazi katika msimu ujao.”

WILBERT MOLANDI NA MUSA MATEJA, DAR

Leave A Reply