The House of Favourite Newspapers

Bosi Juventus: Ronaldo Hauzwi

0

CRISTIANO Ronaldo ataendelea kubaki kuichezea Juventus hadi mwishoni mwa mkataba wake, hivyo ni kwa mujibu wa kigogo wa klabu hiyo.

 

Makamu wa Rais wa Juventus, Pavel Nedved ameyaweka wazi hayo baada ya kuwa na tetesi kuwa Mreno huyo ataondoka mwishoni mwa msimu huu kujiunga na Real Madrid.

 

Ronaldo amekuwa akikosolewa na baadhi ya wachambuzi na mashabiki kwa kutokuwa na msaada kwa timu yake katika michuano ya Ulaya na ile ya Serie A.

 

“Ana mkataba hasi Juni 30, 2022 na ataendelea kuwa nasi,” alisema Nedved na kuendelea:“Kwangu mimi, Cristiano hawezi kuguswa na yeyote katika usajili.

 

Kiongozi huyo ambaye pia ni kiungo wa zamani wa Juventus, na timu ya taifa ya Czech, ameongeza kuwa kocha wa timu hiyo, Andrea Pirlo ataendelea kubaki kuongoza kikosi hicho.

 

“Pirlo ataendelea kuwa kocha wa Juventus, huo ni uhakika asilimia 100,” alisema Nedved

Leave A Reply