BOSI MADAWA YA KULEVYA AHUKUMIWA JELA MAISHA

Image result for el chapo guzman colorado

MLANGUZI wa dawa za kulevya , Joaquin,  maarufu kama El Chapo Guzman, amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kuendesha genge la mauaji ya kihalifu, ambapo sasa amehamishiwa kwenye gereza lenye ulinzi mkali zaidi.

Amehamishwa kwenye gereza lenye ulinzi mkali zaidi lililopo nchini Colorado kwenye ambapo hakuna mfungwa aliyewahi kutoroka.  Gereza hilo lina wafungwa 375 na lilifunguliwa mwaka 1994.

 

Related image

Taasisi ya MCC inayosimamia magereza nchini Marekani imethibitisha taarifa  hiyo na kueleza kuwa ni kutokana na rekodi mbaya ambapo El Chapo Guzman aliwahi kutoroka mara mbili kwenye magereza yenye ulinzi wa hali ya juu  kabla ya kukamatwa tena mwaka 2016..

Julai 17 mwaka huu mtu alihukumiwa kifungo cha maisha jela  baada ya kukutwa na makosa ya biashara ya dawa za kulevya na kushiriki njama za mauaji wakati akiwa kiongozi wa genge kubwa zaidi la biashara hiyo la Sinaloa.


Loading...

Toa comment