Bosi Simba Afunga Mjadala Wa mshambuliaji Wao Mpya Jean Baleke
BAADA ya kuenea kwa taarifa kuhusu usajili wa mshambuliaji wa Simba, Jean Baleke kwamba ametua hapo kwa mkopo akitokea TP Mazembe, uongozi wa Simba umeibuka na kutoa ufafanuzi.
Baleke raia wa DR Congo, amejiunga na Simba katika usajili wa dirisha dogo uliofungwa Januari 15, mwaka huu.
Akizungumza na Spoti Xtra, Meneja wa Habari na mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alifunguka kuwa: “Tetesi au maneno yanayoendelea kuhusu mkataba wetu na Jean Baleke kuwa tumemchukua kwa mkopo sio za kweli.
“Baleke tumemsajili katika dirisha dogo la usajili kwa kandarasi ya miaka miwili kutoka TP Mazembe, kwa hiyo tutakuwa na Belake mpaka 2025.
“Eneo la straika lilikuwa na nafasi moja ya wazi, kwa hiyo tusingeweza kujaza nafasi hiyo kwa kumchukua mchezaji kwa mkopo, Simba hatuna tamaduni hiyo na malengo yetu hayaendani na taratibu hizo.”
STORI: NAILA SHOMARI