The House of Favourite Newspapers

Bosi Simba Atoa Kauli ya Matumaini kwa Mashabiki Wasahau Kipigo Kutoka Yanga

0
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally.

 

MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amewaambia mashabiki wa timu hiyo kuwa, wanatakiwa kusahau matokeo ya Kariakoo Dabi na badala yake wajipange kwa ajili ya michezo ya Ligi Kuu Bara, kwani bado wana kikosi imara.

 

Bosi huyo ameyasema hayo ikiwa ni siku chache baada ya kutoka kufungwa 2-1 dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ngao ya Jamii uliochezwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Akizungumza na Spoti Xtra, Ally alisema: “Wanasimba tumepoteza Kariakoo Dabi, hayakuwa malengo yetu msimu huu, hivyo tutulie na tuungane kwa pamoja tukianza msimu mpya ambao ninaamini unakwenda kuwa mzuri kwetu.

 

“Kama uongozi tunaamini haitakuwa rahisi kusahau, lakini tunapaswa kujisahaulisha maana ligi ndio inaanza, kikubwa tuwaachie kazi benchi la ufundi kwani wao ndio wanatengeneza timu ya ushindi, uzuri ni kwamba tayari wameona upungufu uliopo, hivyo watafanyia kazi yote.”

STORI: WILBERT MOLANDI

Leave A Reply