The House of Favourite Newspapers

Bosi Simba Awazungumzia Kisinda, Morrison

0
Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Aden Rage.

BAADA ya dirisha la usajili la Ligi Kuu Bara kufungwa rasmi Agosti 31 mwaka huu, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Aden Rage amesema kuwa Tuisila Kisinda ataleta upinzani kwenye ligi.

 

Simba na Yanga zimeonyesha kuimarika katika usajili wa msimu huu hasa kuleta wachezaji wenye viwango kutoka nje na wenye majina ambao wanatarajia kuleta ushindani wa hali ya juu msimu ujao.

Simba imesajili wachezaji wanne wa kimataifa ambao ni Larry Bwalya, Bernard Morrison, Chris Mugalu na Joash Onyango, huku Yanga ikiwasajili Tuisila Kisinda, Mukoko Tunombe, Michael Sarpong, Yacoub Sogne na Carlos Stenio ‘Carlinhos’.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Rage alisema kuwa, Simba na Yanga zimefanya mapinduzi makubwa msimu huu kwa kusajili wachezaji nyota wenye majina hivyo ana imani kubwa ushindani utakuwa mkubwa katika ligi msimu ujao.

“Nazipongeza Simba, Yanga na Azam zimefanya usajili mzuri sana kuelekea msimu ujao wa ligi kuu, kwani timu zote zimesajili wachezaji nyota wazuri hivyo naamini msimu ujao kutakuwa na ushindani mkubwa sana kwenye ligi.

“Hii ndio inayotakiwa, ili ligi yetu iweze kuwa bora zaidi ni vyema klabu iwe bora kwa kufanya sajili nzuri kama walivyofanya msimu huu “Kuwepo kwa wachezaji wengi wa kimataifa na wakafanya vizuri inasaidia kuimarisha viwango vya wachezaji wetu wazawa kwani wataona wivu na kujituma zaidi, hivyo kutasababisha timu ya taifa kuwa bora zaidi,” alisema Rage.

Leave A Reply