The House of Favourite Newspapers

Bosi Simba: Yanga Ubingwa Bado

0

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah Muhene ‘Try Again’, amesema kuwa licha ya kushindwa kupata ushindi katika michezo miwili mfululizo ya ligi, bado anaamini kuwa wana nafasi ya kuwa mabingwa na kuwapiku wapinzani wao ambao kwa sasa ndio vinara wa ligi kuu, Yanga.


Simba imeshindwa kupata
matokeo ya ushindi katika michezomiwili mfululizo dhidi ya Mbeya City ambapo walifungwa bao 1-0 jijini Mbeya kisha kutoa sare katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani, juzi Jumamosi.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, kiongozi huyo alisema kuwa licha ya kupoteza pointi muhimu katika michezo yao miwili iliyopita, bado wanayo nafasi kubwa ya kuutetea ubingwa wao kwani bado michezo ni mingi iliyopo mbele yao.


“Wanasimba hawatakiwi kukata
tamaa kwa sasa kwani bado kuna michezo mingi ya kupambania ubingwa, kupoteza pointi au kushindwa kupata ushindi katika michezo miwili iliyopita siyo sababu ya sisi kusema kuwa msimu huu hatuwezi kutwaa ubingwa.


“Kwa sasa tunatakiwa kuangalia
zaidi michezo yetu inayofuata na tuhakikishe kuwa tunakusanya pointi nyingi zaidi, jambo ambalo naamini litatusaidia kuweza kuutetea ubingwa wetu ambao naamini bado upo katika mikono yetu salama,” alisema kiongozi huyo.

STORI: MARCO MZUMBE, Dar es Salaam

Leave A Reply