The House of Favourite Newspapers

Bosi Spoti Xtra Aula TFF

0

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limempa ulaji Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally ambaye ni bosi wa magazeti ya michezo ya kampuni hiyo, Spoti Xtra na Championi, baada ya kumteua katika Kamati ya Habari na Masoko. Kamati hiyo inaongozwa na mwenyekiti, Steven Mnguto, Osuri Kosuri (Makamu Mwenyekiti) na wajumbe wengine ni Cyprian Kuyava, Mgaya Kingoba na Dk. Omar Saleh.

 

Taarifa iliyotolewa na TFF jana Jumatano, ilieleza kuwa, kuna kamati tofauti zimeundwa kutokana na kikao kilichofanyika hivi karibuni ikiwa ni mikakati ya TFF kwa mwaka 2020.

 

Wajumbe walioteuliwa katika Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ni Mwanasheria Elias Mwanjala (Mwenyekiti), Said Soud (Makamu Mwenyekiti), Zakaria Hans Poppe, Issa Batenga, Wakili Msanifu Kondo na Said George. Kamati ya Fedha na Mipango ni Athumani Nyamlani (Mwenyekiti), Francis Ndulane (Makamu Mwenyekiti), Pascal Kihanga, Maxmillian Tabonwa, Paul Bilabaye, Allen Mrindoko, Evans Mgeusa na Seif Muba.

Kamati ya Mashindano ni Ahmed Mgoyi (Mwenyekiti), Saloum Chama (Makamu Mwenyekiti), James Mhagama, Patrick Kahemele, Fortunatus Kalewa, Shafi h Dauda, Sarah Chao, Said Tully na Ali Kamwe. Kamati ya Ufundi ni Vedastus Lufano (Mwenyekiti), Mrisho Bukuku (Makamu Mwenyekiti), Ibrahim Masoud, Ally Mayay, Michael Bundala, Jumbe Menye na Edibily Lunyamila.

 

Kamati ya Mpira wa Vijana ni Khalid Abdallah (Mwenyekiti), Lameck Nyambaya (Makamu Mwenyekiti), Mohamed Aden, Nassib Mabrouk, Salim Kibwana, Vicent Majili, Kenneth Pesambili, Nicky Magarinza na Philip Alando. Kamati ya Waamuzi ni Soud Abdi (Mwenyekiti), Israel Nkongo (Makamu Mwenyekiti), Zahra Mohamed, John Kanyenye na Samwel Mpenzu.

 

Kamati ya Mpira wa Wanawake ni Amina Karuma (Mwenyekiti), Mia Mjengwa (Makamu Mwenyekiti), Rose Kisiwa, Somoe Ng’itu, Zena Chande, Beatrice Mgaya, Sofi a Tigalyoma na Zabibu Juma. Kamati ya Tiba ni Dk. Paul Marealle (Mwenyekiti), Dk. Fred Limbanga (Makamu Mwenyekiti), Dk. Norman Sabuni, Dk. Lisobina Kisongo, Dk. Eliezer Ndama, Dk. Billy Haonga na Dk. Violet Lupondo.

 

Kamati ya Futsal na Beach Soccer ni Blassy Kiondo, Isaac Munisi na Didas Zimbihile. Kamati ya Leseni za Klabu ni Wakili Lloyd Nchunga (Mwenyekiti), Wakili Emmanuel Matondo (Makamu Mwenyekiti), Sunday Kayuni, George Mayawa na Tumaini Mringo.

 

Kamati ya Rufani za Leseni ni Dk. Damas Ndumbaro (Mwenyekiti), Dk. Alex Mgongolwa (Makamu Mwenyekiti), Charles Matoke, David Kivembele na Robert Selasela. Pia Kamati ya Utendaji ya TFF imeunda Kamati ya Maendeleo ya Miradi ili kusimamia utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa vituo vya michezo vya Kigamboni jijini Dar na Tanga.

 

Kabla ya kuunda kamati hiyo, Kamati ya Utendaji ilipokea taarifa ya maandalizi ya utekelezaji wa miradi hiyo kwenye kikao chake kilichofanyika Februari 18, 2020 jijini Dar es Salaam. Wajumbe wa Kamati hiyo ni QS Lucy Mzengi (Mwenyekiti), Mhandisi Hersi Said, Mhandisi Hamad Ramadhan na Mhandisi Charles Adrian.

Leave A Reply