The House of Favourite Newspapers

Bosi Yanga Afichua Kuhusu Tuzo Za Mayele Dhidi ya USM Alger Kwenye Fainali CAF

0
Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe.

AKIWA na mabao 23 kwenye mashindano mawili Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho Afrika, bosi wa Yanga ameweka wazi kuwa mshambuliaji wao, Fiston Mayele anahitaji tuzo zote mbili.

Kwenye ligi, Mayele ni namba moja akiwa amefunga mabao 16 na ametoa pasi mbili za mabao, huku Kombe la Shirikisho Afrika, akitupia mabao sita.

Mayele ni namba moja kwenye Kombe la Shirikisho Afrika sawa na Raga Chivaviro wa Marumo Gallants ambaye timu yake iliondolewa na Yanga hatua ya nusu fainali.

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, amefichua kwamba, Mayele amesema anahitaji kutwaa tuzo zote mbili katika mashindano makubwa msimu huu.

“Mayele anatimiza majukumu yake na furaha yake ipo kwenye kufunga na kuona timu inashinda, ameniambia anahitaji kuchukua kiatu cha ufungaji bora kwenye ligi pamoja na Kombe la Shirikisho Afrika.

“Inawezekana kutokana na kuwa na mechi za kucheza ukizingatia timu imetinga hatua ya fainali, hii ni faida kwa Watanzania wote, hivyo ni muhimu kushirikiana na mashabiki kuzidi kuwa pamoja nasi,” alisema Kamwe.

Yanga itacheza na USM Alger kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu, mchezo wa kwanza Mei 28, 2023 Uwanja wa Mkapa, Dar, marudiano Juni 3, 2023 nchini Algeria.

STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA

#EXCLUSIVE: FEMI wa JUAKALI AMKATAA LUCAS – “WATU WANATAMANI TUOANE, SIJAWAHI KUTAMANI”…

Leave A Reply