The House of Favourite Newspapers

Bosi Yanga SC Ampa Zahera Faili la Niyonzima

Kiungo wa zamani wa Yanga Mnyarwanda, Haruna Niyonzima.

HATIMA ya kiungo wa zamani wa Yanga Mnyarwanda, Haruna Niyonzima ya kurejea Jangwani hivi sasa ipo mikononi mwa Kocha Mkuu Mkongomani, Mwinyi Zahera.

 

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu kiungo huyo atoe ya moyoni kuwa yupo tayari kurejea kukipiga Yanga kama timu hiyo ikihitaji huduma yake kwenye dirisha dogo la usajili.

 

Kiungo huyo hivi sasa anakipiga Klabu ya AS Kigali ya nchini Rwanda baada ya mkataba wake wa kuichezea Simba kumalizika na kuamua kurudi nyumbani kwake kucheza soka.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumamosi na kuthibitishwa na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, jukumu la usajili lipo kwa kocha wao Zahera ambaye ndiye anapendekeza usajili na siyo viongozi.

Mwakalebela alisema kuwa kama kocha akimhitaji kiungo huyo, basi wao hawatakataa mapendekezo yake na badala yake watamsajili kama ilivyokuwa kwenye usajili uliopita.

 

“Tutasikiliza maoni ya kocha kama akitupa mapendekezo yake ya kumsajili, basi kama uongozi hatutasita kumsajili kiungo wetu wa zamani aliyecheza kwa mafanikio muda mrefu.

 

“Ipo wazi Niyonzima ameitumikia kwa kipindi kirefu tangu mwaka 2012 alipojiunga na Yanga, akiwa hapa aliitumika Yanga kwa mapenzi yote na alifurahia uwepo wake katika timu

Comments are closed.