Boss wa Tuzo za Grammy afukuzwa kazi
Boss Wa Tuzo Za Grammy Deborah Dugan amefukuzwa kazi na waendeshaji wa tuzo hizo baada ya kutofautiana kwenye misingi ya kazi. Deborah amelalamika kuwa amefukuzwa baada ya kuonekana kuwa mstari wa mbele ktk kubadilisha tuzo hizo ambazo anadai zinapendelea zaidi wanaume kuliko wanawake na watu weusi.
Pia Deborah anasema kufukuzwa kazi kumetokana na uwamuzi wake wa kutoa siri kuhusu matendo ya unyanyasaji kingono na rushwa kwenye tuzo hizo. Matatizo mengine kwenye tuzo hizo ni pamoja na upendeleo kwenye swala la kupigia kura kazi za wasanii.


