Boti Yapinduka Bahari ya Hindi, Mmoja Ahofiwa Kufa

WATU wamenusurika kifo wakati boti inayomilikiwa na klabu ya starehe ya Yacht jijini Tanga, ilipopinduka jana jioni, Agosti 11, 2019 katika Bahari ya Hindi ikiwa na watu 11 wengi wao wakiwa ni wafanyakazi wa Benki ya NMB Korogwe, ambapo mmoja hajulikani alipo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Edward Bukombe, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

“Baada ya watu hao kupanda boti hiyo wakienda kutembelea visiwa mbalimbali vilivyopo kwenye bahari hiyo ndipo upepo mkali uliwazuia kwenda mbele na walipotaka kugeuza kurudi walipotoka  ilipopinduka na kuwamwaga.

“Kwenye boti hiyo kulikuwa na watu kumi na moja ambapo kumi kati yao waliokolewa kutokana na kuvaa maboya wakati wakiwa baharini na mwingine mmoja ambaye inadaiwa hakuwa nayo hadi sasa hajulikani alipo,” amesema.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi wanaosafiri baharini kuchukua tahadhari kwa kuhakikisha wanavaa maboya ya ili yanapotokea majanga kama hayo waweze kujiokoa.


Loading...

Toa comment