Boxer ndiyo basi tena Yanga

BEKI wa kulia ya Yanga, Paul Godfrey ‘Boxer’ sasa atakuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na majeraha ya goti aliyoyapata Jumamosi iliyopita kwenye mechi dhidi ya Township Rollers ya Botswana.

 

Katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliokuwa na ushindani mkubwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Boxer alikumbana na balaa hilo baada ya kugongana na mshambuliaji wa Township
Rollers wakati wakiwania mpira.

Daktari wa Yanga, Edward Bavu ameliambia Championi Jumatano kuwa, Boxer atakuwa nje ya uwanjani kwa muda mrefu kidogo kutokana na ukubwa wa jeraha hilo.

 

“Hivi sasa (jana asubuhi) tupo njiani tunaelekea mkoani Kilimanjaro, lakini Boxer tumemuacha Dar kwa sababu hali yake bado si nzuri. “Kuna uwezekano mkubwa akawa nje ya uwanja kwa muda mrefu kidogo kutokana na ukubwa wa jeraha hilo alilolipata uwanjani baada ya kugongana na mshambuliaji wa Township Rollers, lakini tunaendelea kupambana ili kuhakikisha anapona haraka.

 

“Kuhusiana na Mapinduzi Balama yeye kwa sasa yupo vizuri kwani siku hiyo aliumia mkono na ulikuwa umevimba ila maendeleo yake ni mazuri na tupo naye,” alisema Bavu.


Loading...

Toa comment