The House of Favourite Newspapers

Bozi: Jina hili alinipa sangoma

0

BOZIGLOBALTVONLINE5Msanii anayefanya vizuri Bongo Movies, Fatuma Ayubu ‘Bozo’

Na Mayasa Mariwata
MSANII anayefanya vizuri Bongo Movies, Fatuma Ayubu amesema jina lake analotumia katika sanaa la Bozi alipewa na Sangoma wakati akihangaika kutafuta matibabu akiwa mdogo.

Akipiga stori na mwandishi wetu, alisema alipokuwa mdogo alisumbuliwa na matatizo mengi yakiwemo ugonjwa wa Pumu, ambayo yalishindikana katika hospitali, hali iliyomfanya kuhangaika kwa waganga wa kienyeji na mmoja wao, alimwambia tatizo lake linatokana na jina lake la Fatuma kumkataa.

“Kuna kipindi kifua kilikuwa kinabana sana, ikawa kama nakandamizwa na kitu kizito, ikawalazimu wazazi wangu kunipeleka kwa sangoma ikaonekana jina limenidhuru ndipo mganga akanipa jina la Bozi, tangu hapo nikawa mzima, ugonjwa wa pumu ukatoweka, nilipoingia kwenye sanaa nikaona ni vyema nikatumia hili jina,” alisema.

Leave A Reply