The House of Favourite Newspapers

Brazil Imekuwa ya Kwanza Kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2018


Brazil imekuwa taifa la kwanza kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia ambazo zitachezewa nchini Urusi mwaka ujao baada ya kuIlaza Paraguay 3-0. 
Brazil chini ya Kocha wao Tite wameshinda mechi zote 9 za michuano hiyo

Hii ina maana kwamba sasa Brazil hawaweza kumaliza chini ya nafasi nne miongoni mwa mataifa ya Amerika Kusini, ambapo mataifa ya kwanza manne ndiyo hufuzu.

Brazil waliwashinda Paraguay kupitia mabao ya mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho, nyota wa Barcelona Neymar na mchezaji wa Real Madrid, Marcelo huku Neymar akikosa mkwaju wa penalti.

Brazil kwa sasa wana alama 9 mbele ya Colombia ambao wanashikilia nafasi ya pili.

Huo ulikuwa ushindi wa nane kwa Brazil chini ya Tite. Paraguay, wana alama chini ya nne bora, zikiwa zimesalia mechi nne kuchezwa.

Argentina wanakabiliwa na kibarua kufuzu baada ya kushindwa 2-0 na Bolivia na kushuka hadi nafasi ya 5, alama moja nyuma ya Chile. Uruguay, walichapwa 2-1 na Peru mjini Lima Jumanne, wapo nafasi ya tatu.

Taifa litakalomaliza nafasi ya tano litacheza mechi mbili za mtoano (nyumbani na ugenini) dhidi ya taifa kutoka Oceania.

Goalkeper: Alisson

Defence: Dani Alves, Marquinhos , Miranda , Marcelo

Midfield: Casemrio/Fernandinho , Paulinho, Renato Augusto

Forwards: Neymar , Coutinho , Gabriel Jesus

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaa, muziki na nyingine kali zikufikie kwa wakati.

Comments are closed.