ACT WAZALENDO YAITAKA SERIKALI KUZALISHA AJIRA KWA VIJANA
CHAMA cha ACT- Wazalendo kupitia Ngome yake ya vijana imesema kuwa inasikitishwa na mwenendo uliopo hapa nchini wa ukosefu wa Ajira mpya na kutokuwepo kwa mazingira rafiki kwa wawekezaji wa ndani hususani kwa vijana.
Akizungumza na waandishi wa habari Katibu wa Sera na Tafiti Ngome ya Vijana ACT-Wazalendo, Kitentya Luth ameiomba serikali kuweka mazingira rafiki katika kuhakikisha vijana waliopo mtaani kwa takribani miaka mitatu bila ajira kupata ajira, na kuwashirikisha katika uzalishaji mali.
Kitentya ameitaka serikali kupitia Waziri wa Viwanda, Waziri wa Ajira, Waziri wa Vijana na Waziri wa Fedha kukaa pamoja ili kutafakari na kuweka mazingira bora kwa wafanyabiashara ndogo katika kuinua uchumi wa nchi na kuchochea Ajira.
Comments are closed.