The House of Favourite Newspapers

Breaking: Arsenal Yamtimua Kocha Mkuu Emery

0

KLABU ya Arsenal leo Ijumaa, Novemba 29, 2019, imemfuta kazi kocha mkuu wake, Unai Emery, baada ya kushindwa kupata ushindi katika michezo saba ya mwisho ya timu hiyo, jambo ambalo halijawahi kutokea tangu 1992.

 

Arsenal imefikia uamuzi huo baada ya jana kupigwa na Frankfurt bao 2-1, kwa mchezo wa saba mfululizo bila ushindi (sare 5 na  vipigo 2).

 

Hata hivyo, Arsenal imemtangaza Freddie Ljungberg kuwa kocha wa muda na kurithi mikoba ya Emery.

 

Mzee Wenger aliitumikia timu hiyo (The Gunners) katika michezo 1,235 lakini hakuwahi kufanya kama alivyofanya Unai. Mara ya mwisho ilikuwa mwaka 1992 chini na mkufunzi George Graham ambaye alisubiri mechi nane mfululizo ndipo apate alama tatu.

Leave A Reply