The House of Favourite Newspapers

Breaking: B12 Wa Clouds Fm Ahamia EFM

0

 

Mkurugenzi wa kituo cha habari cha E Media Tanzania, Francis Ciza ‘Majizzo’ leo Juni 3, 2020 amethibisha kuhamia kwa Mtangazaji maarufu B12 au Dozen katika kituo hicho akitokea Clouds FM.

Kupitia page yake ya Instagram, Majizzo ameandika:
“Nimekuwa kwenye hii tasnia kwa miaka mingi, natambua na kuheshimu mchango wa watu na tasisi zote zilizohusika kutufikisha hapa.

“Lakini majira yanabadilika na kila siku tunahitaji kuongeza nguvu. Kwa sasa nafahamu kwamba @efmtanzania na @tvetanzania, tunaangaliwa sana na vijana kwamba tutaipeleka hii tasnia katika muelekeo wanaotaka. Katika safari hii tunaalika watu wote ambao tunaamini wataunda jeshi imara.
“Hakuna haja ya kueleza kuhusu uwezo na mchango wa Hamisi Mandi @bdozen kwenye hii tasnia. Ni furaha yangu kutangaza kwenu kwamba #Twangala amejiunga na @efmtanzania na @tvetanzania#DozenAmetua”

 

Leave A Reply