The House of Favourite Newspapers

BREAKING: BoT Yakabidhiwa Madini Yaliyokamatwa Yakitoroshwa – Video

Benki kuu ya Tanzania (BOT), leo Juni 29, imekabidhiwa madini, fedha na vito mbalimbali viliyotaifishwa na serikali vilipokuwa vinatoroshwa nje ya nchi, Mawaziri watatu wameshiriki katika zoezi la makabidhiano hayo.

 

WAZIRI WA SHERIA, Dkt. Agustino Mahiga.

“Mwenyezi Mungu alitupa madini mbalimbali tofauti na nchi nyingine miaka ya nyuma hata Mwalimu Nyerere alikua anasema pale Mwadui tumebaki na madini ya miaka saba tu lakini sayansi inasema tuna madini ya zaidi ya miaka 100. 

 

“Tunaambiwa sisi ni masikini lakini ndugu zangu sisi hatuwezi kuwa masikini wakati tuna mali nyingi mno, kuna madini mengine hayajagunduliwa hivyo tuelemishe vijana wetu waweze kuwa na utaalamu wa kuchukua na kuuza madini haya,” amesema Agustino Mahiga.

 

Waziri wa Madini, Dotto Biteko

“serikali ya awamu ya tano imedhamiria kusimamia madini kwa miaka mingi waliokuwa wanachimba wageni hivyo rais ameona uchungu huo na sasa wamepewa watanzania sasa inashangaza unaona eti bado kuna wanaotaka kuiba. Kwa wachimbaji wa madini kama una roho ya madini tafuta kazi nyingine ya kufanya maana ukifanya hivyo utakuwa unatafuta jela au umasikini tunasema sasa basi maana hatutawafumbia macho.

 

“Watanzania tubadilike tuwe taifa la watu waaminifu, lipo kundi linatapeli watu huko je ya nchi sasa ninawaambia siku zenu zinahesabika watu wanakuja kulalamika wanatapeliwa na Watanzania mnatuharibia jina.

 

“Ninawahakikishia watanzania wote kuwa kazi ndo kwanza imeanza tunafanya kila tunachoweza kuhakikisha tatizo hili linakwisha ilikuhakikisha nchi yetu inakwenda mbele na kuwa na mafanikio ya kutosha,” amesema Waziri wa Madini Dotto Biteko.

 

Waziri wa fedha na Mipango Philip Mpango.

“Tukio hili la leo limenifurahisha sana kwani tuna mahitaji mengi sana Watanzania hivyo fedha hizi tutazitumia katika shuguli mbalimbali za kimaendeleo kama vile ujenzi wa barabara, shule, zahanati. Haiwezekani watu wanapo ramali zote hizi, sijui tungejenga Zahanati ngapi kupitia fedha hizi, kuna watu wanalalamika hakuna maji lakini wengine wanapora huu utajiri wetu, sisi sio masikini.

 

“Wanaotuhujumu sasa basi hakuna nafasi tena na niwaombe mahakama na vyombo vya dola msiwe na huruma na hawa watu washughulikiwe kikamilifu kwani hawa ndio wanaorudisha nyuma maendeleo ya nchi yetu. Watanzania wenzangu tusaidie vyombo vyetu vya usalama maana hizi ni mali zetu wote hivyo tuwe macho kuhakikisha tunawaumbua hawa watu wenye nia ovu.

 

“Mali hii iko salama na sisi tunawahakikishia kwamba serikali ikishafanya uamuazi tutatumia mali hii katika kusaidia watanzania, hivyo niwaombe tusaidiane kuhakikisha nchi yetu inakwenda mbele,” Waziri wa fedha na Mipango Philip Mpango.

 

Katibu Mkuu Hazina, Dotto James.

“Kumekuwa na utoroshwaji wa madini ya Tanzanite kwenda nchi jirani halafu wanasema na wao wanayo madini hayo wakati Tanzanite inapatikana Tanzania tu hivyo hatuwezi kuendelea kulifumbia mbacho suala hili,” – Katibu Mkuu Hazina, Dotto James.

 

TAZAMA TUKIO HILO

Comments are closed.