The House of Favourite Newspapers

Breaking: 10 Wafariki Boti Ikizama Ziwa Tanganyika

0

WATU 10 wamefariki dunia na wengine 87 wakiokolewa, baada ya boti iliyokuwa ikitokea maeneo ya Sibosa kupigwa na dhoruba kisha kugonga mwamba na kupasuka kisha kuzama ndani ya Ziwa Tanganyika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, ACP James Manyama, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo katika  Kijiji cha Rufugu wilayani Uvinza na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dhoruba iliyotokana  na upepo mkali katika Ziwa Tanganyika na kusababisha boti kupinduka na kuzama.

 

Aidha Kamanda Manyama amesema kuwa taarifa za awali zinaonyesha kuwa boti hiyo ilikuwa na abiria tisini na saba.

 

Polisi wamesema bado uchunguzi unaendelea ili kubaini kama waathirika wengine wanaweza kupatikana na taarifa juu ya ajali hii zitaendelea kutolewa.

 

Vyombo vya habari nchini humo vinasema,mashuhuda na wakazi wa eneo hilo lililotokea Kijiji cha Sibwesa kuelekea Ikora mkoani Katavi wanasema chanzo cha ajali hiyo ni boti kuwa imejaza kupita uwezo wake na hivyo kusababisha kuzama majini.

Julai 16, mamlaka ya hali ya hewa ilitoa angalizo kuwa kutakuwa na mawimbi na upepo mkali katika ziwa Tanganyika. Mamlaka hiyo ilieleza kuwa hali ya hewa itavuruga shughuli za uvuvi na usafiri wa majini.

 

Mwezi mmoja iliopita ajali kama hii ilitokea katika eneo la kijiji cha Simbwesa ambapo watu tisa walifariki kati ya abiria 60 waliokuwemo katika boti.

 

Leave A Reply