BREAKING: BWENI LATEKETEA KWA MOTO MERU KWA DC MURO – VIDEO

Bweni la Shule ya Sekondari Mlangarini iliyopo katika wilaya ya Meru limeungua moto asubuhi ya leo na kusababisha kuteketea kwa vifaa vya wanafunzi vya shule pamoja na kuungua kwa Vitanda na Magodoro.

Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu, Elisa Palanjo, ameeleza kuwa hakuna mwanafunzi aliyedhurika katika ajali hiyo ya Moto kwa kuwa hakukuwa na Mwanafuzi wakati Moto huo Ulipozuka na kuongeza kuwa chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.

Mkuu wa Wilaya ya Meru, Jerry Muro, alifika eneo la tukio kuwapa walimu na wanafunzi pole na kujionea madhara yaliyojitokeza baada ya tukio hilo.

Loading...

Toa comment