Breaking: CCM Yampitisha Magufuli Kugombea Urais

 

MKUTANO wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, leo Ijumaa, Julai 10, 2020, kwa kauli moja umempitisha  John Magufuli kuwa mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020.

 

“Jumla ya wanachama 32 wamejitokeza kuwania urais (Jamhruri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar) wakiwemo wanawake 5 na wanaume 27, lakini mwanachama mmoja aitwaye Hussein Ibrahim Makungu aliamua kujitoa katika mchakato huo na kubaki wanachama 31.

 

 

“Majina matatu ya wanachama wa CCM yaliyopendekezwa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwenye mchakato wa kuwania urais Zanzibar ni; Khalid Salim Mohammed, Dkt. Husseihn Ally Hassan Mwinyi na Ndg. Shamsi Vuai Nahodha” – Dkt. Bashiru, Katibu Mkuu CCM

 

“Mimi niliomba kura na mzee Pinda na mimi nikampindua, nilikuwa na Makongoro Nyerere lakini leo wote wapo hapa. Sote tuwe kitu kimoja, atakayepatikana ndio tumuunge mkono, maneno mengine yanapitishwa na upinzania na sisi tunayachukua, tusimame na chama chetu.” Rais Magufuli.

 

Aidha, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimezindua rasmi na kuipitisha Ilani yake ya Uchaguzi ya Mwaka 2020 – 2025 leo Ijumaa, Julai 10, 2020, wakati wa Mkutano wa Halshauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dodoma.

 Tecno


Toa comment