BREAKING: CHADEMA Wamshauri Rais! Watu Kutekwa, Kuuawa! – Video

BARAZA la Wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema ) limemtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kukutana na wazee na viongozi wa dini ili kuzungumzia hali ya matukio mbalimbali yanayoendelea hapa nchini ikiwemo utekwaji wa raia na kuuawa.

 

Hayo yameelezwa leo Machi 13, 2018 na Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee wa Chadema Taifa, Roderick Lutembeka wakatia akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar esSalaam ambapo mbali na mambo hayo pia ameeleza wazee hao wanavyoweza kusimama imara na kukemea mwenendo mbaya wa nchi ukiwemo ukiukwaji wa haki za binadamu, katiba na sheria za nchi na matendo mengine maovu.

 

Aidha, Baraza hilo limesema kitendo cha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba kuzungumzia kwamba Kiongozi wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo alijiteka si kitendo cha utu na badala yake angelaani kwa tukio hilo na kuondoa matabaka ndani ya jamii.

 

Stori: Denis Mtima

 

VIDEO: WASIKIE WAZEE WA CHADEMA WAKIFUNGUKA

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment