Breaking: DAS wa Handeni Afariki kwa Ajali, Mbunge Ajeruhiwa

WATU watatu wamefariki dunia akiwemo Katibu Tawala (DAS) wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Mwalimu Boniface Maiga Jumaa baada ya gari mbili kugongana usiku wa kuamkia leo, Jumamosi, Julai 11, 2020, mkoani Dodoma.

Taarifa za awali zinadai kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 7 usku maeneo ya Vikonji Dodoma baada ya gari ka Mbunge wa Handeni, Mhe. Omari Abdallah  Kigoda kugongana na basi aina ya Tata.

 

Imeelezwa kuwa, gari la Mhe Kigoda lilikua na watu wanne akiwemo Mhe. Kigoda mwenyewe, DAS Maiga, dereva na msaidiz wa Mhe. Kigoda.

Ajali hiyo pia imesababisha majeruhi kadhaa akiwemo Mbunge wa Handeni, Mhe.Omary Kigoda. Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Dodoma SACP Gilles Muroto amethibisha.Tecno


Toa comment