The House of Favourite Newspapers

Breaking: Dereva wa Waliomteka Mo Dewji Afikishwa Kortini – Video

DEREVA teksi, Mousa Twaleb (46),  amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumanne Mei 28, 2019, akikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kumteka mfanyabiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji ‘Mo’.   Twaleb amefikishwa mahakama hapo na kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Mo alitekwa na watu wasiojulikana alfajiri ya Oktoba 11, 2018, wakati akifanya mazoezi katika Hoteli ya Colosseum iliyopo jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, alipatikana Oktoba 20 katika eneo la Gymkhana baada ya kudaiwa kutelekezwa na watekaji hao.

Watu 12 walikamatwa na polisi katika tukio hilo wakihusishwa na watekaji. Familia ya Dewji iliahidi kutoa Sh bilioni moja kwa mtu yeyote ambaye angetoa taarifa ambazo zingesaidia kupatikana kwa kijana wao. Hata hivyo, hakuna aliyepata fedha hizo baada ya kupatikana kwake.

Comments are closed.