BAJETI KUU YA SERIKALI YAWASILISHWA BUNGENI – VIDEO

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amewasilisha bungeni bajeti kuu ya Serikali ya shilingi Trilioni 33.1 ambapo amesema serikali imetoa kauli kwamba pato la wastani la kila mtanzania lilifikia TZS milioni 2.4 mwishoni mwa mwaka jana kutoka TZS milioni 2.3 mwaka 2017.

Kwa mujibu wake, ongezeko hilo ni sawa na wastani wa asilimia 5.6.

 

Miongoni mwa masuala makuu aliyoyasema katika hotuba yake ni yafuatayo:

”Nimpongeze Rais Magufuli kwa uthubutu na uzalendo mkubwa ambao umewezesha kutekelezwa kwa miradi mbalimbali mikubwa ya maendeleo na nimshukuru kwa kuendelea kuniamini kusoma bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2019/20. Kama kuna tuna tuzo au nishani napendekeza kamati ya bajeti iwe kamati ya kwanza kukabidhiwa tuzo hiyo, kwa kuboresha makadirio ya bajeti 2019/2020. 

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango akionyesha Mkoba unaowakilisha Bajeti Kuu ya Serikali alipowasili katika viwanja vya Bunge leo jijini Dodoma tayari kwa ajili ya kuwasilisha Mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. Serikali imewasilisha mapendekezo ya shilingi trilioni 33 kwa ajili ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2019/2020.

“Bajeti ya 2018/2019 Serikali ilitarajia kupata Tril. 32.48 hadi April 2019, mapato ya kodi yalifikia tri 12.9, mapato yasiyo ya kodi Tril 2.04 na mapato yasiyokuwa ya kodi yalivuka lengo kwa sababu ya kuimarika kwa matumizi ya teknolojia. Kutofikiwa kwa lengo la kukusanya mapato ya kodi kulitokana na ugumu wa kutoza kodi kwa sekta isiyo rasmi, mwamko mdogo wa wananchi kudai risiti za kietroniki wanapofanya manunuzi.

 

“Katika mwaka wa fedha wa 2018/19 jumla ya shilingi Bilioni 616.9 zimetumika kugharamia elimu bure ya shule za msingi na mikopo ya elimu ya juu. Hadi April 2019 Serikali imetoa Tril 5.4 kwa ajili ya miradi ya maendeleo Tril. 4.89 ni fedha za ndani na bilioni 500 ni fedha za nje, kiasi hiki hakijumuishi baadhi ya fedha kutoka kwa washirika wa maendeleo.

 

“Katika bajeti ya mwaka 2018-2019 serikali ilitarajia kupata jumla ya shilingi Trilioni 32.48 kutoka katika vyanzo vyote vya ndani na nje, mchanganuo wa mapato yaliyopatikana hadi April, 2019 ni Trilioni 12.9 sawa na 87.4%. Mnamo mwaka 2018/19 maeneo yaliyopatiwa fedha ni mishahara kwa watumishi ni Tril. 6.3 zimelipwa, madeni ya Serikali Tril. 5.7, kuendeshaji wa ofisi tril. 4, mradi Umeme Rufiji Bil. 723.6 elimu bure na mikopo ya wanafunzi Bil 616, ununuzi wa ndege Bil. 200.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango akiwasilisha Hotuba ya Mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 leo jijini Dodoma. Serikali imewasilisha mapendekezo ya shilingi trilioni 33 kwa ajili ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2019/2020.

“Kati ya mwezi Julai 2018 na Aprili 2019, Serikali imegharamia miradi na matumizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Trilioni 6.3 ya mishahara, Trilioni 5.7 ya madeni ya nchi na Bilioni 616.9 ya Elimu bure na Mikopo ya Elimu ya Juu. “Napendekeza kutoza ushuru wa bidhaa wa asilimia 10 kwenye nywele za bandia zinazotengenezwa nchini na asilimia 25 kwenye nywele bandia zinazoagizwa kutoka nje ya nchi, lengo la hatua hii ni kuongeza mapato ya Serikali.

 

“Napendekeza kuongeza muda wa leseni za udereva kutoka miaka mitatu ya sasa hadi miaka mitano, napendekeza kuongeza tozo ya leseni ya udereva kutoka Tsh. 40,000 kwenda Tsh. 70,000. Mafanikio yaliyopatikana kwa miaka mitatu ni ukuaji wa pato la taifa kwa asilimia 6.6, kukua kwa Sekta ya Kilimo asilimia 5.3, kudhibiti mfumuko wa bei kwa tarakimu moja, kupungua kwa kiwango cha umaskini kutoka kwa asilimia 28.2 hadi asilimia 26.4.

 

“2015/16 kulikuwa na Mashirika 13 tu Serikali yaliyotoa gawio kwa Serikali na yalitoa Bil.119, sasa yameongezeka hadi mashirika 28 mpaka Mei 2019 yametoa gawio la Bil. 497.5. “Kati ya kipindi cha Julai 2018 na Aprili 2019 Serikali imetumia Bilioni 232.8 kununua ndege kwa ajili ya Shirika la Air Tanzania, ambapo ndege za Boeing 787-8 Dreamliner na Bombadier Q400 zitawasili nchini mwishoni mwa mwaka huu 2019.

“2019/2020 tutaboresha mazingira ya kufanya baishara ili kuvutia uwekezaji, kupanua wigo wa kodi na kuongeza mapato ya Serikali, kurekebisha viwango vya kodi na kulinda viwanda vya ndani dhidi ya viwanda vya nje. Serikali itapunguza kiwango cha kodi kwa umeme unaouzwa kutoka Tanzania kwenda Zanzibar kutoka kwa asilimia 18, hadi 0 ili kuwapunguzia gharama za maisha kwa wananchi wa Zanzibar.

 

“Kuna mafanikio katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi, Ripoti ya Uwazi ya Kimataifa mwaka 2018 imeonesha Tanzania kuwa nafasi ya 16 kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ikilinganishwa na nafasi ya 27 mwaka 2015. Napenda kuwasisitiza tena watumishi wa TRA kwamba hairuhusiwi kufunga biashara ili kushinikiza mfanyabiashara alipe kodi au malimbikizo ya kodi isipokuwa kwa kibali cha Kamishna Mkuu wa TRA.

 

“Serikali itapunguza kiwango cha kodi kwa umeme unaouzwa kutoka Tanzania kwenda Zanzibar kutoka kwa asilimia 18, hadi 0 ili kuwapunguzia gharama za maisha kwa wananchi wa Zanzibar. Kufuta kwa msamaha kodi ya ongezeko la thamani kwenye taulo za kike kwa kuwa haujawezesha kupatikana kwa bei nafuu kwa bidhaa hiyo muhimu kwa walengwa, badala yake ni kuwanufainisha wafanyabiashara.

Baadhi ya Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wa Wizara mbalimbali wakifuatiliana Hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango akiwasilisha Hotuba ya Mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 leo jijini Dodoma.

“Shabaha za uchumi jumla katika kipindi hiki ni kukua kwa Pato la Taifa kwa 7.1% mwaka 2019 kutoka ukuaji halisi wa 7.0% mwaka 2018, Mfumuko. Shabaha za uchumi jumla katika kipindi hiki ni kukua kwa Pato la Taifa kwa 7.1% mwaka 2019 kutoka ukuaji halisi wa 7.0% mwaka 2018, mfumuko wa bei kubaki kati ya 3.0% hadi 4.5% pamoja na mapato ya ndani kufikia 15.8%.

 

“Napendekeza kusamehe kodi ya ongezeko la thamani kwenye makasha yenye majokofu yanayotumika kwenye kilimo cha kisasa cha mboga mboga kwa wakulima watakaoingiza makasha hayo kutoka nje ya nchi kwa matumizi ya kilimo. Napendekeza kutoza ushuru wa asilimia 35 badala ya 25 kwa mwaka mmoja kwenye bidhaa za sausage na zinazofanana na hizo, pia kutoza kodi ya asilimia 35 badala ya 25 kwa nyanya zilizosindikwa (Tomato Sauce).

 

“Napendekeza kuongeza muda wa leseni ya udereva kutoka miaka 3 hadi 5, kuongeza tozo ya leseni 40,000 hadi 70,000, ada ya usajili wa magari 10,000 hadi 50000, bajaji kutoka 10,000 hadi 30,000 na pikipiki kutoka 10,000 hadi 20,000. Napendekeza kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye makasha yenye majokofu yanayotumika kwenye kilimo cha kisasa cha mboga mboga kwa wakulima watakaoingiza makasha hayo kutoka nje ya nchi kwa matumizi ya kilimo.

Katibu Mkuu Kiongozi (kushoto) na Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mizengo Pinda wakisoma vitabu vya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 wakati ikiwasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango (hayupo pichani) leo Bungeni jijini Dodoma. Serikali imewasilisha mapendekezo ya shilingi trilioni 33 kwa ajili ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2019/2020.

“Kwa upande wa misaada na mikopo nafuu kutoka nje, Serikali itaendelea kuzungumza na Washirika wa Maendeleo ili kila upande uzingatie misingi na kanuni za ushirikiano.

 

“Shabaha zingine za Serikali ni kuongeza mapato ya kodi hadi kufikia 13.1% ya Pato la Taifa kutoka 12.1%, matumizi ya Serikali kufikia 22.7% kutoka 21.6% na nakisi ya Bajeti inakadiriwa kufikia 2.3% ya Pato la Taifa kutoka 2.0% ya mwaka 2018/19.

 

“Napendekeza kutoa msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa vilainishi vya ndege vinavyoingizwa nchini, tiketi za ndege, vipeperushi, kalenda, shajara, karatasi zenye nembo na sare za wafanyakazi zilizowekwa nembo ya Shirika. Bajeti ya mwaka wa fedha wa 2018/19 iliyoidhinishwa na Bunge ilikuwa Tsh. trilioni 32.48 ambapo Tsh trilioni 20.47 ni matumizi ya kawaida na Sh trilioni 12.01 ni matumizi ya maendeleo.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akipitia kitabu cha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 wakatiikiwasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango leo Bungeni jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba na Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso. Serikali imewasilisha mapendekezo ya shilingi trilioni 33 kwa ajili ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2019/2020.

“Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kulipa madai yaliyohakikiwa na kuchukua hatua mbalimbali kwa lengo la kupunguza walimbikizaji wa madai na kuhimiza uzingatiaji wa sheria ya bajeti namba 11 ya 2015. Jumla ya Shilingi Tril 33.11 zinatarajiwa kukusanywa na kutumika katika bajeti ya mwaka 2019/20. Mapato ya ndani ni Tril 23.05 ambayo ni 69.6% ya bajeti yote. Mapato yatakayotokana na kodi ni Tril 19.10 sawa na asilimia 12% ya pato la taifa.

 

“Tozo zote zilizokuwa zinatozwa kwa dola za Kimarekani zitatozwa kwa shilingi ya Tanzania, isipokuwa kwa shehena za kemikali zinazokwenda nje ya nchi. Napendekeza kufutwa kwa ada ya matumizi ya maji kwa watumiaji wenye visima nyumbani ambayo ilikuwa inatozwa kuanzia Shilingi 100,000 na kuendelea kulingana na matumizi ya maji.

 

“Wananchi wataruhusiwa kutoa mizigo yao bandari bila ulazima wa kutumia Mawakala ili kupunguza gharama kwa wananchi, lakini mizigo inayokwenda nje itaendelea kuhudumiwa na Wakala. Serikali imeanzisha kitengo kipya cha kupokea malalamiko ya kodi na kitaratibiwa na Wizara ya Fedha na Mipango, kitahusisha kupokea malalamiko kutoka kwa walipa kodi yakiwamo ya kuombwa rushwa na Watumishi wa Mamlaka ya Kodi TRA.”

FUATILIA TUKIO ZIMA HAPA


Loading...

Toa comment