Breaking: Ishu Ya Chama Yatinga TFF, Kuamuliwa na Kamati Ya Sheria
UONGOZI wa klabu ya Simba umepeleka barua kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuishitaki Yanga kwa kuvunja kanuni za usajili. Simba wamefi kia maamuzi hayo mara baada ya Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela kufunguka kuwa wamefanya mazungumzo na kiungo wa Simba, Clatous Chama juu ya kutaka kumsajili mchezaji huyo.

