The House of Favourite Newspapers

BREAKING: Ishu ya MO Dewji, Serikali Yamjibu LEMA – Video

Serikali imesema inao uwezo wa kuchunguza uhalifu wa aina yoyote nchini kwa kutumia vyombo vyake vya ndani ikiwemo Jeshi la Polisi na kukanusha kushindwa kufanya uchunguzi na upelelezi wa uhalifu unaotokea nchini yakiwepo matukio ya utekaji kama alivyosema Mbunge Godbless Lema wakati akizungumza na wahabari jijini Dar es Salaam leo.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, mbele ya Mkutano wa waandishi wa habari baada ya kikao na Maafisa wa Jeshi la Polisi Visiwani Zanzibar..

 

Wakati huo huo Naibu Waziri Masauni, amemuaguiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuwachukulia hatua Maafisa wa Askari walioshindwa kutekeleza agizo alilolitoa mwanzoni mwa mwaka huu lakuletwa mbwa maalumu atakaetumika kukagua mizigo ili kudhibiti Dawa za Kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.

 

Awali leo mchana, Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) na Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani, Godbless Lema, alisema serikali inao wajibu mkubwa wa kuleta wachunguzi wa kimataifa kwa ajili ya kufanya upelelezi wa tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji (Mo) na watu wasiojulikana Alhamisi iliyopita, Oktoba 11, 2018 katika eneo la Hoteli ya Colosseum eneo la Oyster Bay jijini Dar es Salaam.

VIDEO: FUATILIA TUKIO HILO HAPA

Comments are closed.